Sudan yamkamata kiongozi wa jaribio la uasi
2021-09-22 08:41:29| CRI

Sudan yamkamata kiongozi wa jaribio la uasi_fororder_src=http___www.xinhuanet.com_photo_2021-09_21_1127886292_16322291896661n&refer=http___www.xinhuanet

Baraza la Usalama na Ulinzi nchini Sudan jana Jumanne lilitangaza kukamatwa kwa Meja Jenerali Abdul-Baqi Hassan Osman, ambaye ni kiongozi wa jaribio la uasi.Baraza liliongeza kuwa maofisa wengine 22 wa kijeshi wa ngazi tofauti, maofisa kadhaa wasiopewa majukumu na askari pia walikamatwa.

Baraza hilo liliitisha mkutano wa dharura, ulioongozwa na mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan, kujadili hali ya usalama nchini humo kufuatia jaribio la uasi.

Waziri wa ulinzi wa Sudan Yassin Ibrahim Yassin amesema kupitia taarifa kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa jaribio hilo la uasi lililenga kunyakua madaraka na kuhujumu mchakato wa sasa wa mpito.