Tamasha la sita la vijana wa China na Afrika lafunguliwa Beijing
2021-10-20 10:24:07| CRI

Tamasha la sita la vijana wa China na Afrika lafunguliwa Beijing_fororder_111

Tamasha la sita la vijana wa China na Afrika lilifunguliwa jana tarehe 19, Oktoba hapa Beijing, likipambwa na wimbo uliopigwa kwa ala za jadi za Kichina.

Akizungumza kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa tamasha hilo lililohudhuriwa na vijana 45 kutoka nchi 44 za Afrika, msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Deng Li amewataka vijana wa China na Afrika kutumia ipasavyo nafasi yao muhimu katika kuzidisha maelewano kati ya watu wa pande hizo mbili na kutoa injini kubwa kwa maendeleo ya uchumi na ushirikiano kati ya China na Afrika.

Balozi wa Nigeria nchini China Baba Ahmad Jidda kwenye hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya video alipongeza miaka 100 ya kuzaliwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China CPC na mafanikio ya China katika kutokomeza umaskini uliokithiri. Amesema katika hali mpya ya sasa, vijana wa Afrika na China wanapaswa kubeba wajibu na kushirikiana kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya Afrika na China.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Soong Ching Ling wa China Bw. Wang Jiarui ametoa hotuba akiwakaribisha vijana wa Afrika kueleza maarifa yao waliyopata nchini China kwa jamaa na ndugu zao, na kuwahamasisha watu wengi zaidi wa Afrika kujiunga kwenye shughuli za kuhimiza urafiki kati ya China na Afrika.

Akiwa kwa niaba ya vijana wa China, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing Lin Zhiyuan alihutubia ufunguzi wa tamasha hilo akisema, vijana wa China wanapenda kufahamu tamaduni za kiafrika na pia kupenda kueleza hadithi za kichina kwa wenzao wa Afrika. Naye mwanfunzi wa Cameroon anayesoma katika Chuo Kikuu cha Peking JOSEPH olivier MENDOO alielezea barua mbili alizomwandikia rais Xi Jinping wa China na barua alizojibiwa na rais Xi. Alisema vijana wa Afrika wanaoishi China wanapenda kueneza urafiki kati ya China na Afrika, na kushirikiana pamoja na vijana wa China ili kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika.

Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Senegal, ambapo pande mbili zitatangaza hatua mpya za ushirikiano zinazolingana na maendeleo na mahitaji ya kila upande. Katika siku za baadaye, vijana wa China na Afrika watakuwa na fursa nyingi zaidi za kuonesha vipaji vyao.