Rais Xi Jinping wa China afanya ukaguzi mkoani Shandong
2021-10-21 21:29:12| CRI

Rais Xi Jinping wa China afanya ukaguzi mkoani Shandong_fororder_94e4ec8032f9408db4eca6366faa0887

Rais Xi Jinping wa China tarehe 20 alitembelea sehemu ya Mto Huanghe kuingia baharini katika mji wa Dongying, mkoani Shandong.

Wakati wa ziara hiyo, alikwenda gati ya Mto Huanghe kuingia baharini, Kituo cha Ufuatiliaji wa hali ya ikolojia kwenye Delta ya Mto Huanghe, Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Delta ya Mto Huanghe, kukagua hali ya maji kwenye Mto huo na hali ya ikolojia ya eneo hilo, ili kupata ufahamu kwa kina juu ya ulinzi wa kiikolojia ya Bonde la eneo la mtiririko wa Mto Huanghe na maendeleo ya kiwango cha juu.

Siku kadhaa kabla ya hapo, rais Xi alitoa hotuba kwenye Mkutano wa viongozi wa Mkutano wa 15 wa Nchi Zilizosaini Mkataba wa Anuwai ya Viumbe (COP15), akisisitiza kuwa ili kuimarisha uhifadhi wa viumbe anuwai, China inaharakisha mchakato wa ujenzi wa mfumo wa hifadhi za mazingira ya asili, na kuyahusisha maeneo yenye mifumo muhimu ya ikolojia, mandhari ya kipekee ya asili, urithi bora wa asili, na viumbe anuwai kwenye mfumo huo.