China yatoa mwongozo wa kufikia kilele na kusawazisha caboni chini ya falsafa mpya ya maendeleo
2021-10-25 09:42:44| cri

China yatoa mwongozo wa kufikia kilele na kusawazisha caboni chini ya falsafa mpya ya maendeleo_fororder_中国减排头图

Mamlaka za China jana Jumapili zilizindua waraka wenye mwongozo wa kazi ya kufikia malengo ya kilele cha utoaji caboni na usawazishaji wa caboni chini ya falsafa mpya ya maendeleo, na kuweka shabaha maalumu na hatua katika miongo ijayo.

Mwongozo huo umebainisha kuwa hadi kufikia mwaka 2030 utoaji wa caboni nchini China utafikia kilele, utakuwa tulivu kisha utapungua, na hadi kufikia mwaka 2060 China itasawazisha utoaji wa caboni na kutokuwa na uchafuzi kabisa, kuwa na caboni chache na uchumi wa mzunguko.

Waraka huo uliotolewa kwa pamoja na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la Serikali, umeelezea kazi kuu tano, zikiwemo kujenga mazingira yasiyokuwa na uchafuzi, caboni chache na uchumi wa mzunguko, kuboresha ufanisi wa nishati, kuongeza kiwango cha matumizi ya nishati zisizokuwa za visukuku, kupunguza utoaji wa caboni na kupiga jeki uwezo wa kuzamisha caboni wa mifumo ya ikolojia.