Waziri Mkuu wa Sudan arejea nyumbani akiwa chini ya ulinzi mkali
2021-10-27 09:15:35| cri

Waziri Mkuu wa Sudan arejea nyumbani akiwa chini ya ulinzi mkali_fororder_苏丹头图

Ofisi ya waziri mkuu nchini Sudan imeeleza kwenye mtandao wake wa facebook kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdalla Hamdok amerejea nyumbani na mke wake wakiwa chini ya ulinzi mkali.

Awali ofisi hiyo Jumanne ililitaka jeshi la Sudan kuwaachilia huru maafisa wote wanaoshikiliwa. Kamanda Mkuu wa jeshi hilo Abdel Fattah Al-Burhan Jumanne aliapa kufikia mpito wa kidemokrasia na kulinda azimio la Disemba. Amesisitiza kuwa wanataka kusahihisha njia ya mpito na walichofanya sio mapinduzi ya kijeshi, aidha amewahakikishia watu kuwa serikali ijayo itakuwa ya kiraia tu na kujumuisha watendaji wenye uwezo na haitashirikisha wafuasi wa upande wowote.

Kamati Kuu ya Madaktari wa Sudan imesema takriban watu wanane wameuawa na wengine 157 kujeruhiwa Jumatatu wakati askari wakiwatawanya waandamanaji huko Khartoum.