Xinjiang ni sehemu yenye uhuru na ustawi
2021-11-02 15:27:32| CRI

图片默认标题_fororder_微信图片_20211029141209

Xinjiang ni mkoa mkubwa zaidi unaojiendesha wa makabila madogo madogo nchini China, na una wakazi zaidi ya milioni 25 wa makabila karibu 50, wakiwemo Wauyghur. Katika miaka ya hivi karibuni, suala la Xinjiang limechukuliwa na baadhi ya nchi za magharibi kama njia ya kupaka matope China. Ili wageni wajue zaidi hali halisi mkoani humo, Chuo Kikuu cha Beijing hivi karibuni kiliwapeleka wanafunzi 20 kutoka Burundi, Uganda, Uingereza, Marekani, Australia, Russia, Mongolia, Korea Kusini, Pakistan na nchi nyingine kutembelea miji kadhaa ya mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang, ikiwemo Kashgar, Hotan, na Urumqi. Bw. Pierre Gacira kutoka Burundi ni mmoja wao, na baada ya kutembele Xinjiang aliandika makala ili kueleza aliyoyaona mkoani humo.

 

Kwenye makala yake, Pierre amesema kabla ya hapo, alikuwa anapata habari za Xinjiang kupitia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, magazeti, au hotuba za kisiasa. Mitandao na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vimejaa ripoti za watu wa makabila madogo mkoani Xinjiang haswa Wauyghur kukabiliwa na mateso ya kidini, kulazimishwa kufanya kazi, na kupotoshwa mawazo. Amesema ziara hii ni fursa nzuri kwake kuchunguza ukweli moja kwa moja, na kuthibitisha kama ripoti hizo ni za kweli. Alikuwa na shauku ya kutaka kujua kiwango cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi mkoani Xinjiang, kama kuna misikiti, na kama waumini wa dini ya Kiislamu wana uhuru wa kuabudu. Pia alitaka kutembelea vituo vya mafunzo ya ufundi stadi kuona kinachoendelea huko, na kuwasiliana na watu wa makabila madogo huko ili kufahamu maisha yao ya kila siku.

Huko Kashgar, walitembelea Msikiti wa Aitgaer wenye historia ya miaka 500, ambao vyombo vya habari vya Magharibi vilisema umebomolewa na serikali ya China. Imamu Maimat Juma alituambia kwamba, msikiti huo uliwahi kushambuliwa na magaidi, na baba yake aliuawa katika shambulizi hilo. Alisema Rais Xi Jinping wa China alitembelea hapo na kuagiza serikali kutoa fedha kwa mradi wa ukarabati wa msikiti huo.

Siku ya pili, walitembelea Kituo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi. Ugaidi umekuwa changamoto ya kimataifa, katika nchi ya Pierre Burundi, mara nyingi imekumbwa na mashambulizi ya kigaidi. anatumai kwamba kupitia ziara hii, anaweza kujifunza kuhusu uzoefu wa China katika kuondoa itikadi kali. Kituo alichotembelea ni kama eneo kubwa la ujasiriamali, ambapo wanafunzi huko wanajishughulisha na upandaji miti ya matunda, na ufugaji wa mifugo ikiwemo kuku, mbuzi, kondoo, na ng'ombe. Hii ni kama shule ya elimu ya ufundi stadi, na wanafunzi watagawiwa sehemu ya mapato ya kituo hicho kutokana na kazi zao za ujasiriamali baada ya kuhitimu. Kijana mnufaika wa kituo hicho Muhammad aliwaambia kwamba, aliacha itikadi kali, na kununua gari kwa kutumia fedha alizopata hapo, na sasa yeye ni dereva wa taksi.

Huko Hotan, walitembelea Chuo cha Kiislamu cha Xinjiang, ambacho ni chuo kikubwa kinachovutia wanafunzi wengi kutoka nchi jirani, na pia kimeajiri walimu kutoka Saudi Arabia, Pakistan, Misri na nchi nyingine, na wanatumia Quran kuwafundisha wanafunzi. Pierre amefurahi sana kuona Quran ikinukuliwa na wanafunzi wa China. Mkuu wa chuo hicho Abdurekev Tumuniyazi aliwaambia kuwa, serikali kuu ya China imetoa misaada muhimu ya fedha na rasilimali kwa kazi za kufundisha na ibada ya wanafunzi. Pia imesaidia kujenga msikiti, ukumbi, mabweni, bwalo na miundombinu mingine. Serikali kuu ya China pia inatoa bima ya matibabu na elimu ya lazima kwa watu wa makabila madogo madogo mkoani Xinjiang, ili kuhakikisha maisha na maendeleo yao.

Kwenye makala yake, Pierre amesema kuna methali inayosema, ‘Kusikia sio Kuona’, ni kwa kushuhudia tu kwa macho yako mwenyewe unaweza kujua ukweli. Huko Xinjiang, dini za Kiislamu, Kikristo na Buddha zinastawi, na tofauti za kitamaduni na kidini huvutia watalii zaidi ya milioni 20 kila mwaka. Ameona hali inayotofautiana kabisa na ripoti potofu za baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi. Watu wa Xinjiang wanafurahia uhuru kikamilifu katika maisha ya kijamii, kidini na kiutamaduni.