China yatoa waraka juu ya maendeleo ya demokrasia ya Hong Kong chini ya sera ya “nchi moja, mifumo miwili”
2021-12-20 14:56:26| Cri

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China leo imetoa waraka uliopewa jina la “Hong Kong: Maendeleo ya Demokrasia chini ya Utaratibu wa Nchi Moja, Mifumo Miwili”.

Waraka huo uliobainisha mapitio ya kina kuhusu asili na maendeleo ya demokrasia ya mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong na misingi na nafasi ya serikali kuu, umesema chini ya utawala wa kikoloni wa Muingereza hakukuwa na demokrasia. Aidha umeelezea kuwa baada ya kurejesha mamlaka, serikali ya China ilitekeleza sera ya msingi ya“nchi moja, mifumo miwili”, kuanzisha demokrasia katika mkoa huo, na tokea hapo imekuwa ikitoa uungaji mkono endelevu kwenye mkoa huo katika kuendeleza mfumo wake wa demokrasia. Nia, udhati na juhudi za Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na serikali ya China hadi sasa bado vimeendelea kuwa imara na hata kwa waangalizi wasio na upendeleo.

Waraka huo pia umesifu sera ya “nchi moja, mifumo miwili” kama uvumbuzi wa kiubunifu wa CPC na serikali ya China ambao umethibitisha kuwa una mafanikio makubwa mkoani Hong Kong.