Shehena ya tano ya msaada wa chanjo ya COVID-19 ya China yawasili Zimbabwe
2021-12-21 08:33:04| CRI

Shehena ya tano ya msaada wa chanjo ya COVID-19 ya China yawasili Zimbabwe_fororder___172.100.100.3_temp_9500033_1_9500033_1_1_03378754-785c-418b-bead-6628da7d0513.JPG

Shehena ya tano ya msaada wa chanjo ya COVID-19 kutoka kampuni ya Sinovac ya China imewasili Harare, mji mkuu wa Zimababwe jana mchana.

Makamu wa rais ambaye pia ni waziri wa afya wa Zimbabwe Constantino Chiwenga amepokea chanjo hizo kwenye uwanja wa ndege kwa niaba ya serikali ya Zimbabwe. Bw. Chiwenga ameishukuru China kwa kutoa msaada na uungaji mkono wa pande mbalimbali kwa Zimbabwe katika kupambana na COVID-19.

Naye Balozi wa China nchini humo Bw. Guo Shaochun amesema, msimamo wa China wa kuunga mkono nchi za Afrika kupambana na COVID-19 na kuhakikisha usalama wa watu wa Afrika ni thabiti na wazi. Ameongeza kuwa, kama ikihitajika, China itaendelea kutoa msaada wa chanjo kwa nchi za Afrika mpaka bara hilo litakaposhinda vita dhidi ya COVID-19 kikamilifu.