Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya mfanyakazi wa shirika la kibinadamu nchini Sudan Kusini
2021-12-21 08:53:53| CRI

Kaimu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Matthew Hollingworth amelaani shambulizi lililolenga msafara wa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja huo (WFP) lililotokea jumapili kati ya Tindiir na kijiji cha Duk Padiet, mkoa wa Jonglei na kusababisha kifo cha mfanyakazi wa shirika hilo na mwingine kujeruhiwa.

Hollingworth amesema, wafanyakazi hao walikuwa wakitokea Tindiir, ambako walipeleka msaada muhimu wa chakula kwa watu walioathiriwa na mafuriko wakati watu wenye silaha walishambulia kwa risasi msafara huo.

Tukio hili linafanya idadi ya wafanyakazi wa kibinadamu waliouawa wakiwa kazini kwa mwaka huu kufikia watano.