Polisi nchini Uganda yasema kundi jipya la waasi linawajibika na mauaji ya askari polisi
2021-12-22 08:14:44| CRI

Jeshi la Polisi nchini Uganda limesema kundi jipya la waasi linawajibika na mauaji ya askari polisi kadhaa yaliyotokea katikati ya nchi hiyo.

Msemaji wa Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu nchini humo Charles Twiine amesema, kundi la watu wenye uhusiano na Muungano wa Nguvu ya Mabadiliko ya Uganda walikamatwa na polisi na kukiri kuhusika na mauaji hayo.

Twiine amesema, watu hao walisema wameandikishwa kutoka maeneo ya Wakiso na kukiri kuwaua askari polisi katika maeneo ya Busunju na Kibongo mwezi huu. Pia amesema, bunduki mbili za polisi zilizoibwa kutoka kwa askari polisi zimepatikana na watuhumiwa wanane wamekamatwa.