Kikosi cha askari wa miguu wa kulinda amani wa China chawasili Juba
2021-12-22 10:32:06| CRI

 

 

     Kundi la pili la askari 350 wa miguu wa kulinda amani wa China jana wamewasili mjini Juba, nchini Sudan Kusini, na askari wote 700 wa kundi hilo wamepangwa na kuanza kutekeleza majukumu ya muda wa mwaka mmoja.

     Kikosi hicho kitatekeleza majukumu ya doria ya kutumia silaha, kufanya msako, kufanya ulinzi wa kujikinga na kuwalinda raia. Wakati wa kukamilisha majukumu ya ulinzi wa amani, askari hao pia watashiriki kwenye msaada wa matibabu, maingiliano ya utamaduni na uokoaji wa kibinadamu.