Huawei kupeleka vifaa vya kidijitali kuboresha uhifadhi wa wanyamapori barani Afrika
2021-12-23 08:56:21| CRI

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya China, Huawei, imesema itapeleka teknolojia yake ya 5G ili kuboresha uhifadhi wa spishi maarufu za wanyamapori barani Afrika, huku kukiwa na matishio yanayohusiana na vitendo vya kibinadamu na mabadiliko ya tabianchi.

Kampuni hiyo imesema, teknolojia yake ya 5G na kamera za kisasa zitasaidia usimamizi wa wanyamapori katika maeneo yao ya asili katika kanda ya Afrika kusini mwa Sahara.

Pia vifaa hivyo vya kidijitali vya kampuni hiyo zitasaidia kupiga picha za wanyama na kuzituma kwa wakati, kuepuka hatari zinazoweza kutokea, na pia kudumisha sekta ya utalii katika bara hilo.