Nchi 22 za Afrika zaripoti kesi za virusi vya Omicron
2021-12-24 08:49:13| cri

Nchi 22 za Afrika zaripoti kesi za virusi vya Omicron_fororder_VCG111359425664

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Afrika CDC) jana kimesema kuwa nchi 22 za Afrika zimeripoti kesi za virusi vya COVID-19 vilivyobadilika aina ya Omicron.

Mkurugenzi wa Afrika CDC Bw. John Nkengasong amesema, katika wiki iliyopita, nchi sita za Afrika zikiwemo Burkina Faso, Togo, Misri, Kenya, Morocco na Mauritius zimeripoti kesi za virusi vya Omicron, na kuongeza kuwa virusi hivyo vinaenea kwa kasi barani Afrika.

Umoja wa Afrika (AU) hivi karibuni ulionya kuwa marufuku ya  kusafiri kutokana na kuongezeka kwa kesi za Omicron imezuia usafirishaji wa watu na bidhaa, na kuleta athari kubwa kwa nchi za Afrika.