Rais wa Kenya asifu barabara ya mwendokasi iliyojengwa na China na kusema ni mradi muhimu wa miundombinu
2021-12-24 08:45:49| CRI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesifu barabara ya kasi ya Nairobi iliyojengwa na kampuni ya CRBC ya China na kusema ni mradi muhimu wa miundombinu.

Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 27.1, rais Kenyatta amesema barabara hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa magari ulioshuhudiwa ambao pia uliongeza gharama za kufanya biashara nchini humo, na pia itachukua nafasi kubwa katika kuboresha ushindani na kupunguza gharama za kuishi katika nchi hiyo.

Amemsifu mkandarasi wa China kwa kufanya kazi nzuri na kueleza imani yake kuwa barabara hiyo itakamilika na kuwa tayari kutumika itakapofika mwezi Machi mwaka ujao.