DRC yatangaza kumalizika kwa mlipuko wa homa ya uti wa mgongo
2021-12-24 08:45:14| CRI

Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jena-Jacques Mbugani ametangaza kumalizika kwa mlipuko wa homa ya uti wa mgongo katika maeneo ya Banalia, mkoa wa Tshopo ulioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Amesema mlipuko wa homa ya uti wa mgongo uliotangazwa mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, umesababisha vifo vya watu 205 kati ya watu 2,662 waliougua homa hiyo.

Waziri huyo ametangaza kumalizika kwa mlipuko hiyo baada ya kutokuwepo na ripoti za maambukizi kwa wiki kadhaa, na kiwango cha maambukizi kushuka na kufika chini ya mstari wa tahadhari kwa muda wa wiki mbili mfululizo.