Ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” waongezeka kati ya Januari na Novemba mwaka huu
2021-12-24 08:44:35| CRI

Ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” waongezeka kati ya Januari na Novemba mwaka huu_fororder_VCG111157527457

Takwimu mpya zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zimeonyesha kuwa, ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeendelea kuongezeka kati ya Januari na Novemba mwaka huu, na kuwa moja ya mambo muhimu katika uwekezaji wa China katika nchi za nje.

Takwimu zinaonyesha kuwa, uwekezaji wa moja kwa moja usio wa kifedha wa China umefikia dola za kimrekani bilioni 100.5, na thamani ya kandarasi zilizokamilika nchi za nje imefikia dola za kimarekani bilioni 134.4.

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, kati ya Januari na Novemba, uwekezaji wa China katika nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeongezeka kwa asilimia 12.7 kuliko mwaka jana, na thamani ya kandarasi zilizokamilika nchi za nje imefikia dola za kimarekani bilioni 76.65, ikiongezeka kwa asilimia 8.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo.