22: Urithi

Hekalu la Tiantan

Ukitembelea Beijing usikose kutembelea Ukuta Mkuu, Kasri la Kifalme, Summer Palace na Hekalu la Tiantan, kwa sababu majengo hayo yanawakilisha kiwango cha juu kabisa ufundi wa majengo ya kale ya China. Hekalu la Tiantan lilijengwa kwa ajili ya wafalme kuomba mavuno mazuri na amani.

Hekalu la Tiantan lilijengwa mwaka 1420, ni mahali pa kufanyia tambiko kwa wafalme wa enzi mbili za Ming na Qing. Hekalu hilo liko kusini ya Kasri la Kifalme la Beijing, na eneo lake ni mara nne kuliko Kasri la Kifalme la Beijing. Majengo muhimu katika sehemu ya hekalu hilo yako katika upande wa kusini na kaskazini, na kuna madhabahu moja ya duara. Madhabahu ya duara ina matabaka matatu ya ngazi, na kila tabaka lina ukingo wa mawe. Madhabahu hayo yalijengwa kwa ajili ya wafalme kufanyia matambiko.

Jengo jingine muhimu ni hekalu la kuombea mavuno mazuri. Ni jumba lenye matabaka matatu ya upenu na lilijengwa juu ya jukwa lenye matabaka matatu ya ngazi. Mafundi seremala wa China ya kale kwa akili zao, walijenga hekalu hilo kwa mbao tupu bila misumari. Mwaka 1998 hekalu hilo liliorodheshwa na UNESCO kwenye kumbukumbu za urithi wa utamaduni wa dunia.

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14