22: Urithi

Kasri la Potala

Kasri la Potala liko mjini Lahsa katika mkoa wa Tibet, kasri hilo linasifiwa kama ni lulu iliyoko kwenye paa la dunia.

Kasri la Potala ni mahali pa msufii wa dini Buddha madhehebu ya Tibet kufanya shughuli za siasa, mambo ya dini na kuishi. Kasri hilo lilianza kujengwa katika karne ya 7, lakini katika karne ya 9 kasri hilo liliharibika na kuachwa kutokana na miaka mingi ya vita.

Mwaka 1645 kasri la Potala lilijengwa upya, kazi ya kujenga kasri hilo ilichukua miaka 50, na baadaye lilipanuka na kujengwa zaidi. Kasri hilo lina ghorofa 13, urefu wa mita 110, ni jengo la mawe na mbao. Katika karne kadhaa kasri lilipitia matetemeko ya ardhi, lakini bado liko imara. Kasri hilo lilitumia dhahabu kilo 3724 na lulu 15000. katika karne ya 17 kasri hilo lilipopanuliwa, wachoraji wakubwa wa Tibet walichora picha zaidi ya elfu kumi kwenye kumbi, milango na kuta. Picha hizo nyingi zilichorwa kwa mujibu wa hadithi za kihistoria na za dini, ni vitu vya sanaa vyenye thamani kubwa katika kasri hilo. Ndani ya kasri la Potala, kumehufadhiwa picha, sanamu za mawe, za mbao na sanamu za ufinyanzi. Na pia vimehifadhiwa vitu vingi vya kauri, vikionesha historia ndefu ya maingiliano ya kirafiki kati ya kabila la Watibet na Wahan. Mwaka 1994 kasri la Potala liliorodheshwa na UNESCO katika urithi wa Dunia.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14