22: Urithi

Sokwe wa Beijing (Peking Man)

Magharibi ya Mji wa bejing kilomita 48, kuna kijiji kimoja milimani, kinachojulikana kama Zhou Kuo Dian. Kijiji hicho si kikubwa, upande wake wa kaskazini magharibi ni milima, na upande wake wa kusini masharini ni eneo kubwa lenye rutuba mpaka upeo wa macho. Ndani ya kijiji, kuna milima miwili nidogo ambayo ni milima ya mawe ya chokaa. Milimani kuna pango kubwa lenye urefu wa mita 140, mwaka 1929 ndani ya pango hilo vitu vya watu wa kale viligunduliwa.

Mwaka 1921 mwnasayansi kutoka Sweden na mwaka 1927 mwanasayansi kutoka Canada waligundua meno mawili ya binadamu wa kale. Mwaka 1929 mtaalamu wa mambo ya kale Pei Wenzhong aligundua fuvu kamili la Sokwe wa Beijing kutoka udongo mwekundu.

Kwenye Zhou Kou Dian ugunduzi uliendelea kufanyika katika muda wa miaka 80. Vitu vilivyogunduliwa kutoka huko vilikuwa ni kisukuku, vyombo vya mawe, na visukuku vya wanyama wanyonyao maziwa.

Ndani ya pango hilo pia yaligunduliwa majivu yenye unene wa mita 6, majivu hayo yamedhihirisha wazi kuwa nyani-mtu wa Beijing walikuwa wametumia moto.

Karibu na pango hilo viligunduliwa vyombo vya mawe elfu kumi kadhaa, vyombo hivyo vimeonesha kuwa watu waliotumia vyombo hivyo walikuwa katika Kipindi cha Vyombo vya Mawe.

Watu hao waliotumia vyombo hivyo, walikuwa miaka lake 4 hadi 3 iliyopita.

Tokea hapo, kijiji cha Zhou Kou Dian kilianza kuvuma duniani kutoka kwenye ukimya wa awali. Wataalamu wa mambo ya kale walichukulia kijiji hicho kama kituo cha kuchunguza chanzo cha binadamu jinsi walivyoishi kabla ya miaka kiasi cha laki 4 iliyopita. Mwezi Desemba mwaka 1987, UNESCO iliorodhesha kwenye urithi wa dunia.

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14