Rais Zuma ailipa serikali dola milioni 7.8 za ukarabati uliofanywa kwenye nyumba yake binafsi
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameilipa serikali dola za kimarekani milioni 7.8 za ukarabati uliofanywa kwenye nyumba yake binafsi.
Malipo hayo ameyafanya kutokana na maagizo yaliyotolewa na mahakama ya kikatiba. Msemaji wa Rais Bongani Ngqulunga amesema Rais Zuma alikusanya fedha hizo kupitia mkopo wa benki ya Mutual.
Mahakama hiyo ilimuamuru Zuma mwezi machi mwaka huu kulipia ukarabati uliofanywa ambao hauhusiani na usalama wa rais.
Zaidi ya dola milioni 17 zinadaiwa kutumika kwenye ukarabati huo katika makazi ya Zuma yaliyoko Nkandla, KwaZulu Natal.
Baada ya uchunguzi kufanywa na afisa wa kulinda mali za umma Thuli Madonsela ilibainika kwamba Zuma alifaidika kinyume cha sheria na ukarabati huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |