Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani asema NATO inahitaji kuzungumza na Russia
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw. Frank-Walter Steinmeier amesema, NATO inahitaji kuzungumza na Russia.
Kauli hiyo ya Bw. Steinmeier aliitoa alipokutana na wenzake wa Latvia, Lithuania, na Estonia jana huko Riga, Latvia, ambapo walibadilishana maoni kuhusu usalama na ulinzi wa Ulaya, utekelezaji wa azimio la mkutano mkuu wa Warsaw wa NATO, na pia uhusiano kati ya NATO na Russia. Baada ya mkutano huo, Bw. Steinmeier alisema, ingawa msukosuko wa Ukraine bado haujatatuliwa kikamilifu, lakini ni lazima mazungumzo kati ya NATO na Russia yadumishwe na kupanuliwa.
Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Latvia Bw. Edgars Rinkevics alisema sasa mazingira ya kuanza mazungumzo na Russia si mazuri, na kama mapambano hayatasimamishwa kote nchini Ukraine, basi hakuna uwezekano wa kuondoa vikwazo walivyoweka dhidi ya Russia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |