• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 10-Septemba 16)

    (GMT+08:00) 2016-09-16 16:34:49

    Katibu mkuu na mwenyekiti wa Baraza Kuu la UN walaani vikali jaribio la nyuklia la Korea Kaskazini

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwenyekiti wa Baraza Kuu la umoja huo Mogens Lykketoft wamelaani vikali jaribio la nyuklia lililofanywa na Korea Kaskazini, na kuihimiza nchi hiyo isimamishe mpango wake wa nyuklia.

    Katibu mkuu Ban amesema kitendo hicho cha Korea Kaskazini kinakwenda kinyume na maazimio husika ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kinahatarisha amani na usalama wa kikanda. Bw. Ban pia ameitaka Korea Kaskazini ibadilishe mwelekeo wake na kuazimia kuachana na nyuklia.

    Naye mwenyekiti Lykketoft kwenye taarifa yake anasema amesikitishwa sana na "kitendo hicho cha kutowajibika wala kukubalika" ambacho kinaletea matishio makubwa kwa amani na usalama wa kimataifa. Ametoa wito kwa Korea Kaskazini kuachana na mpango wa silaha za nyuklia na makombora, na kutekeleza majukumu yake ya kimataifa.

    Habari zaidi zinasema kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema litachukua mara moja hatua stahiki juu ya kitendo hicho, na kuandaa azimio jipya.

    Korea Kaskazini ilifanya jaribio la bomu la nyuklia ijumaa wiki iliyopita, ikiwa ni mara ya tano kwa nchi hiyo kufanya majaribio ya nyuklia tangu mwaka 2006.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako