China imefanikiwa kurusha maabara ya anga za juu ya Tiangong-2
China imefanikiwa kurusha maabara ya anga za juu ya Tiangong-2 Alhamisi saa 4:04 usiku kwenye Kituo cha Kurusha Satilaiti cha Jiuquan, kaskazini magharibi mwa China.
Tiangong-2 itaingia kwenye njia ya mzunguko iliyo kilomita 393 juu ya sayari ya dunia, ambako kituo cha baadaye cha anga za juu cha China kitafanya kazi.
Chombo cha anga za juu cha Shenzhou-11 kitakachobeba wanaanga wawili wa kiume kwenye anga za juu kitarushwa baadaye ili kuungana na maabara hiyo katikati hadi mwishoni mwa mwezi ujao. Wanaanga hao watafanya kazi kwenye Tiangong-2 kwa siku 30 kabla ya kurudi kwenye sayari ya dunia
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |