Waziri mkuu wa serikali ya Scotland Bibi Nicola Sturgeon amesema Scotland itatoa mswada mpya wa kura za maoni kuhusu uhuru wa nchi hiyo. Wizara hiyo inasema hatua hiyo inalenga kulinda maslahi ya Scotland baada ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya. Bibi Sturgeon amesema Scotland ina haki ya kufikiria kujitenga kutoka Uingereza, kama mustakbali wake ikiwa sehemu ya Uingereza si mzuri, na itamaliza kura za maoni kabla ya Uingereza kujitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya.
Na huku hayo yakijiri Waziri mkuu wa Uingereza Bibi. Theresa Mary May amesema bunge la Uingereza litakuwa na haki ya kushiriki kikamilifu kwenye mjadala kuhusu suala la Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, kauli ambayo inamaanisha kuwa serikali ya Uingereza imelikubali bunge kujiunga na mchakato huo.
Bibi Theresa May amesisitiza kuwa bunge halipaswi kuizuia Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |