Kiongozi wa waasi DRC ajisalimisha baada ya miaka 5
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kiongozi wa kivita ambaye alikua bado hajapatikana tangu kutoroka kwake kutoka gerezani mwaka 2011 alijisalimisha kwa viongozi wa mkoa wa Lubumbashi Jumanne wiki hii, kusini mwa nchi hiyo.
Gédéon Kyungu alikua akionogza kundi la waasi la 'Bakata Katanga', wanamgambo ambao jina lake katika Kiswahili sanifu linamaanisha "kuigawa Katanga", mkoa wa kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Pamoja na watu wake, Bw Kyungu alikua akiendesha harakati zake kusini mwa nchi, ambapo makundi ya wanamgambo walishambulia raia na kuwapora mali zao na rasilimali za madini.
Gédéon Kyungu alikuwa alikamatwa na kuhukumiwa mwaka 2009 mjini Lubumbashi, mji wa pili wa nchi hiyo, kufuatia hukumu kwa uhalifu dhidi ya binada.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |