Umoja wa Afrika wafikiria kutoa fidia kwa raia walioathiriwa na operesheni za vikosi vyake nchini Somalia
Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imesema imeanza mchakato wa kuwalipa fidia raia walioathiriwa na operesheni zake nchini Somalia.
Hii ni mara ya kwanza kutokea barani Afrika, kwa wahanga kulipa fidia kutokana madhara yaliyotokana na watumishi wa AMISOM.
Ofisa anayeshughulikia mambo ya sera za maendeleo wa Umoja wa Afrika Bw Jide Okeke, amesema hatua hiyo itasaidia kuboresha uhusiano kati ya AMISOM na wenyeji.
Hatua hii imefikiwa baada ya mkutano kuhusu mwenendo wa kawaida wa operesheni, wenye lengo la kuratibu utendaji wa idara mbalimbali za AMISOM.
Makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano huo yatawasilishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya kupitishwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |