Ethiopia yatangaza hali ya hatari
Serikali ya Ethiopia imetangaza hali ya hatari kwa kipindi cha miezi sita kufuatia ghasia na mauaji ambayo yameendelea kwa miezi kadhaa.
Jamii ya watu wa Oromo na Amhara ambao ni asilimia 60% ya watu wote wamekuwa wakiandamana wakidai kwamba jamii ya Tigre ndio inayoshika karibu nyadhifa zote serikalini.
Akitangaza hali hiyo ya hatari waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn alisema "serikali inaweka mbele usalama wa wananchi"
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |