Afrika Kusini imeanzisha mchakato wa kujiondoa kutoka uanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.
Wanadiplomasia wa Afrika kusini wamearifu umoja wa mataifa juu ya uamuzi huo na kuilaumu ICC kwa kuzilenga zaidi nchi za Afrika.
Baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kujiondoa katika uanachama wa Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Hatua hii ya Afrika Kusini inakuja siku nne baada ya rais wa Burundi kusaini sheria ya kuindoa nchi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita.
Uamuzi wa Afrika kusini kujiondoa ulitokana na shinikizo iliokumbana nazo mwaka uliopita za kuitaka imkamate rais wa Sudan Omar al Bashir wakati wa mkutano wa muungano wa nchi za Afrika mjini Johannesburg.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |