Jeshi la Iraq mbioni kuikomboa Mosul
Jeshi la Iraq linaendelea na mapambano yake makali kuurejesha mji wa Mosul ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo, kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State.
Makamanda wa jeshi la Iraq wanasema wameudhibiti tena mji wa Bartella, ulioko karibu na Mosul.
Hata hivyo, wapiganaji pia wamekuwa wakijibu mapigano kwa kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga ya bomu ya kutegwa ndani ya gari kabla ya kuzidiwa.
Wapiganaji hao wa Islamic State pia wanadaiwa kukishambulia na kulipua kiwanda cha kemikali kusini mwa Mosul.
Shambulio hilo ambalo pia lilifanywa kiwandani mwaka 2003, na kusababisha moto kuwaka kwa wiki kadhaa, limesababisha kutanda hewani gesi chafu ya salfa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |