Uganda kurefusha muda wa uwepo wa jeshi lake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuisaidia kupambana na kundi la waasi
Jeshi la Uganda limesema litarefusha muda wa uwepo wa jeshi lake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa miezi kadhaa kutokana na ombi la Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya.
Msemaji wa jeshi la Uganda Luteni Kanali Paddy Ankunda amesema Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya wamezitaka nchi za Afrika Mashariki zirefushe kwa mwaka mmoja muda wa vikosi vyao vinavyoshiriki kwenye juhudi za kulitimua kundi la LRA kutoka nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |