Trump asema atakubali matokeo ya kura ya Urais ikiwa atashinda
Mgombea wa urais wa Marekani kupitia tiketi ya chama cha Democrat Donald Trump amesema kuwa atakubali matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani iwapo atashinda.
Amesema kuwa atakubali matokeo ya moja kwa moja yasio na udanganyifu wowote akiongezea kuwa ana haki ya kupinga matokjeo hayo iwapo hayatakuwa na utata.
Alionekana katika mkutano mjini Delaware jimbo la Ohio, akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya mjadala wa tatu wa urais dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton.
Bwana Trump amekuwa akikosolewa kwa kusema kuwa hatakubali matokeo ya uchaguzi huo.
Donald Trump alikataa kuahidi kukubali matokeo ya uchaguzi iwapo atashindwa, katika mjadala wa mwisho wa urais dhidi ya Hillary Clinton.
Kura za kutafuta maoni zinaonyesha Trump poteza umaarufu katika majimbo makuu baada ya kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |