Zika yagunduliwa Tanzania
Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, nchini Tanzania NIMR inasema imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini humo.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela, anasema wiki hii kwamba virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.
Dkt Mwele Malecela amesema kwamba kwa sasa serikali inaangazia kuzuia wajawazito wasiumwe na mbu ambao wanaaminika kueneza virusi hivyo.
Hata hibvyo anasema bado wanajaribu kuangalia ni aina gani ya virusi vya Zika.
Virusi vya Zika zimekuwa vikisababisha watoto kuzaliwa wakiwa na ubongo uliodumaa na vichwa vidogo katika mataifa ya Amerika Kusini na sana Brazil.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |