Watu watatu wajeruhiwa baada ya gari lililotegwa bomu kulipuka nchini Somalia
Gari lililotegwa bomu limelipuka kwenye mgahawa mmoja ulio karibu na ikulu ya mjini Mogadishu, Somalia, na kusababisha kifo cha mshambuliaji na watu wengine watatu kujeruhiwa.
Msemaji wa manispaa ya Mogadishu Abdifitah Omar Halame amesema, lengo la mshambuliaji huyo lilikuwa ni kuua watu wengi zaidi, lakini hakufanikiwa kutokana na juhudi zilizofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.
Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulizi hilo, lakini kundi la Al Shabaab limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini humo dhidi ya serikali.
Hali ya usalama imeimarishwa mjini Mogadishu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais tarehe 28 mwezi huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |