Jeshi la Nigeria lawaokoa mateka 605
Jeshi la Nigeria limewaokoa watu 605 waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram kwenye msitu wa Sambisa.
Kamanda wa operesheni ya Lafiya Dole Bw. Lucky Irabor amesema mjini Maiduguri kuwa kati ya waliookolewa, kuna wanaume 69, wanawake 180, wavulana 227 na wasichana 129 katika operesheni hiyo iliyofanyika kati ya tarehe 7 na tarehe 14 Desemba.
Kwa sasa mateka waliokolewa wanalindwa na jeshi la Nigeria, kwa ajili ya uchunguzi na kuhojiwa baadaye.
Doria zinazofanywa na jeshi la Nigeria zimesaidia kuokolewa kwa mateka wengi, na kuuawa kwa wapiganaji wengi wa kundi la Boko Haram.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |