Misri yatuhumu viongozi wa kundi la Muslim Brotherhood kuhusika na mlipuko uliotokea kanisani
Wizara ya mambo ya ndani ya Misri wiki hii imewatuhumu viongozi wa kundi la Muslim Brotherhood waliokimbilia Qatar kwa kutoa mafunzo na kufadhili watu waliofanya shambulizi kwenye kanisa moja mjini Cairo ambapo watu 25 waliuwawa.
Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema, uchunguzi umebaini kuwa, viongozi wa kundi hilo walioko Qatar walitoa ufadhili, vifaa na maelekezo kwa mtu aitwaye Mohab Moustafa el Sayed Qassim kutoa mafunzo na kufanya mashambulizi hayo.
Kundi la Muslim Brotherhood limekanusha kuhusika kwa namna yoyote na mlipuko uliotokea wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa linalopakana na Kanisa Kuu la Mtakatifu Marko.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |