Rais Barack Obama wa Marekani amesema hakuna uhusiano wa pande mbili wenye umuhimu mkubwa zaidi kuliko uhusiano kati ya Marekani na China, na kama uhusiano huo ukivunjika, kila mmoja ataathirika.
Obama ameyasema hayo alipokuwa akitoa hotuba yake ya mwisho wa mwaka na kusema uhusiano kati ya Marekani na China ni muhimu kwa uchumi wa dunia na usalama wa kitaifa
Rais mteule wa Marekani, Donalda Trump mapema mwezi huu alipokea simu kutoka kwa Kiongozi wa Taiwan, Tsai Ing-wen, baada ya mawasiliano hayo, ikulu ya Marekani ilisisitiza tena kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja.
Inatambuliwa na jumuiya ya kimataifa kuwa kuna China moja tu duniani, na zote bara na Taiwan ziko ndani ya China moja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |