Polisi nchini Uturuki yawatambua washukiwa wawili wa milipuko ya mabomu nchini humo
Polisi nchini Uturuki imewatambua washukiwa wawili, mmoja akiwa mwanamke, wanaotuhumiwa kuhusika katika milipuko miwili ya mabomu iliyotokea katikati ya mji mkuu wa nchi hiyo, Istanbul Jumamosi iliyopita, ambapo watu 44 waliuawa na wengine 155 kujeruhiwa.
Gari lililotumika kwenye mashambulizi hayo lilinunuliwa kupitia mtandao wa internet na kupelekwa kwa washukiwa hao na mtu mwingine.
Wapiganaji wa kundi la Kurdistan Freedom Hawks, ambalo ni tawi la kundi la PKK, wamekiri kuhusika na shambulizi hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |