Putin na Netanyahu wajadili ushirikiano wa kukabiliana na ugaidi katika Mashariki ya Kati
Rais Vladmir Putin wa Russia na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamejadili kwa njia ya simu hali ya Mashariki ya Kati na mapambano dhidi ya ugaidi
Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Russia imesema, viongozi hao wamethibitisha utayari wao wa kuongeza ushirikiano zaidi wa vitendo katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Jumatano iliyopita, Netanyahu alituma salamu za rambirambi kufuatia mauaji ya balozi wa Russia nchini Uturuki Andrei Karlov.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |