Askari wa kulinda amani wa China warudi kutokea Sudan Kusini
Kikosi cha pili cha askari wa kulinda amani wa China waliokwenda nchini Sudan wamerejea baada ya kumaliza majukumu ya miezi 12 ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Kikosi hicho kilifanya kazi mbalimbali zikiwemo kufanya doria kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa na kulinda maeneo ya raia. Kikosi hicho pia kilipewa medali ya heshima ya amani na Umoja wa Mataifa.
Julai 8, Koplo Li Lei na Sajengi Yang Shupeng waliuawa katika mapigano yaliyotokea kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kati ya vikosi vya serikali na askari wanaomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Kikosi cha tatu cha askari wa kulinda amani kiliondoka China mapema mwezi huu na kinatekeleza majukumu yao nchini Sudan Kusini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |