Marais wa China na Zimbabwe wakutana
Rais Xi Jinping wa China wiki hii amekutana na rais Robert Mugabe wa Zimbawe mjini Beijing.
Katika mazungumzo yao, rais Xi amesema kuwa China inaishukuru Zimbabwe kwa kuiunga mkono katika masuala makubwa yanayofuatiliwa na maslahi muhimu ya China.
Pia amesisitiza kuwa China inapenda kuhimiza viwanda vyenye uwezo mkubwa vya China kuwekeza nchini Zimbabwe, na kupanua ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Naye Rais Mugabe ameeleza matumaini ya nchi yake ya kukuza ushirikiano kati yake na China katika sekta za miundo mbinu na mambo ya kilimo.
Mwaka 2015 China na Zimbabwe zilisaini mikataba ya miradi ya thamani ya dola bilioni 4 katika sekta za Kilimi, uchumbaji madini, kawi na maendeleo ya miundo mbinu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |