Maendeleo madogo yapatikana kwenye mchakato wa amani Darfur
Kiongozi wa tume ya Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Darfur Bw Herve Ladsous amesema maendeleo madogo yamepatikana kwenye mchakato wa amani katika jimbo la Darfur, na ametoa wito wa ufumbuzi wa kudumu unaowawezesha wakimbizi milioni 2.6 wa ndani warudi makwao au kutafuta makazi mapya.
Akitoa ripoti kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Darfur, Bw. Ladsous amesema raia bado wanakabiliwa na matishio ya kiusalama yanayotokana na mgogoro wa kikabila na uhalifu, ikiwemo shughuli za wanamgambo wenye silaha.
Lakini mapigano kwenye eneo hilo yamepungua kidhahiri kutokana na hatua za kijeshi zilizochukuliwa na serikali ya Sudan dhidi ya makundi ya waasi, na juhudi za serikali za kupunguza vurugu za kikabila.
Bw. Ladsous ametoa wito wa kutafuta ufumbuzi wa muda mrefu wa kutatua suala la wakimbizi wa ndani milioni 2.6 na kuondoa vyanzo vya mapigano ya kugombea ardhi, maji na maliasili nyingine.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |