Ujerumani kupeleka helikopta nane na askari 350 wa ziada nchini Mali
Serikali ya Ujerumani imepitisha wiki hii uamuzi wa kupelekwa kwa helikopta nane na askari 350 wa ziada nchini Mali ikiwa ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini humo.
Ndege hizo, ambazo ni pamoja na helikopta za kivita na zile ambazo zitatumiwa kwa usafiri wa askari, zitachukua nafasi ya zile za Uholanzi.
Baada ya kupelekwa kwa ndege hizo, uamuzi ambao utapitishwa na bunge la Ujerumani, Ujerumani itakua na askari 1,000 nchini Mali, kwa jumla ya askari 15,000 wa kikosi cha kulinda amani kiliyotumwa nchini humo.
Jukumu la Umoja wa Mataifa ni kusimamia mkataba wa amani ulioafikiwa mwaka 2015 kati ya serikali ya Mali na waasi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |