Obama awaaga Wamarekani kwa hotuba iliyojaa hisia
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho kabla ya kuondoka madarakani Januari 20.
Obama amechangua mji wa Chicago alikoanzia harakati zake za kisiasa kutoa hotoa yake hiyo ambapo amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia, na kuahidi kuendeleza utamaduni wa Marekani wa kukabidhi mamlaka kwa njia ya amani.
Katika hotuba yake ya saa moja, rais Obama aliorodhesha mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa utawala wake wa miaka minane, ikiwemo kudhibiti kushuka kwa uchumi, kufungua ukurasa mpya na Cuba, kusainiwa kwa makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran, na kuongeza upatikanaji wa bima ya afya.
Ametaja changamoto kubwa tatu zinazoikabili Marekani, ambazo ni ukosefu wa usawa wa kipato, ubaguzi wa rangi, na mgawanyiko wa kisiasa, na kuwataka wananchi wa Marekani kukubali wajibu wao kama wananchi.
Rais Obama mwenye umri wa miaka 55 na ambaye ndiye Rais wa Kwanza mweusi wa Marekani amehudumu kwa vipindi viwili.
Wakati akimpongeza mkewe Mitchell na binti zake Sasha na Malia Obama alibubujikwa ma machozi akiwataja kama nguzo muhimu zaidi kwenye kipindi chake cha Urais.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |