Ahmad Ahmad, kutoka Madagascar achaguliwa rais mpya wa shirikisho soka Afrika
Ahmad Ahmad, kutoka nchini Madagascar amechaguliwa kuwa Rais mpya wa shirikisho la kandanda barani Afrika.
Ahmad alipata kura 34 na kumshinda Issa Hayatou ambaye ameongoza shirikisho hilo la CAF kwa muda wa miaka 29.
Matokeo hayo yamepokelewa na shangwe katika baraza la Caf huku Ahmed akibebwa katika mabega na wafuasi wake na kumpeleka mbele ya jukwaa baada ya matokeo kutangazwa.
Ahmad ,ambaye alikuwa rais wa shirikisho la soka nchini Madagascar mwaka 2003, anachukua urais wa Caf katika kipindi cha miaka 4 na ameahidi kulifanya shirikisho hilo kuwa la kisasa mbali na kuweka uwazi.
Kazi yake ya kwanza ,alisema awali siku ya Alhamisi kwamba itakuwa kuzindua sheria mpya za maadili huku akisema kuwa maafisa wa soka wa Afrika watachunguzwa maadili yao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |