Viongozi wa China na Saudi Arabia wakubaliana kinua zaidi uhusiano kati ya nchi zao
Rais Xi Jinping wa China wiki hii mjini Beijing amefanya mazungumzo na mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia.
Viongozi hao wamekubaliana kudumisha mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Saudi Arabia, kusukuma mbele ushirikiano katika pande mbalimbali, na kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.
Rais Xi Jinping amesema China inaunga mkono Saudi Arabia kutimiza "dira ya mwaka 2030", na inaipongeza Saudi Arabia kuwa mwenzi wa China katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kupenda kuwa mwenzi wa kiuchumi wa Saudi Arabia.
Baada ya mazungumzo yao, wakuu hao wameshuhudia kusainiwa kwa nyaraka mbalimbali za ushirikiano wa sekta za uchumi, nishati, uzalishaji wa kiviwanda, utamaduni, elimu na sayansi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |