Chama cha VVD chashinda viti vingi katika Baraza la chini la bunge la Uholanzi
Chama cha kiliberali cha VVD nchini Uholanzi kinachoongozwa na waziri mkuu wa sasa Bw. Mark Rutte kimeshinda kwa viti 31 kati ya viti 150 katika Baraza la chini la bunge la Uholanzi, na kudumisha nafasi yake ya uongozi.
Chama cha mrengo wa kulia PVV kinachopinga uislamu, uhamiaji na Umoja wa Ulaya kilipata viti 19 tu.
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa serikali ya awamu mpya inatakiwa kuundwa kwa vyama visivyopungua vinne.
Kwenye kampeni vyama vyote vikubwa vimesisitiza kwamba havitashirikiana na chama cha PVV kwenye serikali ya muungano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |