• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (27 Mei-2 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-02 20:48:37

    Zaidi ya watu 80 wauwawa kwenye mlipuko Kabul

    Watu wasiopungua 80 wameuawa na wengine zaidi ya mia tatu kujeruhiwa Jumatano, katika shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari mjini Kabul nchini Afghanistan, wanasema polisi.

    Walioshuhudia wanasema waliskia mlipuko mkubwa na baadaye wingu la mosi kuonenakana likitanda kwenye eneo la karibu na makazi ya wanadiplomasia.

    Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo.

    Nyumba zilizokuwa jirani na bomu hilo lilipolipuka pia zilipatwa na madhara kwa madirisha na milango kupasuka.

    Mwezi uliopita wapiganaji wa Taliban walitangaza kuanza kufanya mashambulizi na kusema kuwa yatakuwa yanalenga majeshi ya kigeni.

    Na kwingineko Watu wasiopungua 24 wameuawa na wengine 100 kujeruhiwa Jumatano katika mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotokea mjini Bagdad, Iraq.

    Shambulizi la kwanza lilitokea usiku wa tarehe 29, ambapo mshambuliaji wa kujitoa mhanga alilipua gari lililokuwa na mabomu katika makazi ya waumini wa dhehebu la Shia na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 13. Shambulizi lingine lilitokea karibu na daraja la al-Shuhadaa na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 11.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako