• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (27 Mei-2 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-02 20:48:37

    Serikali ya Nigeria yaanza kuwarudisha maisha ya kawaida wasichana wa Chibok waliookolewa

    Serikali ya Nigeria imesema kazi ya kuwarudisha kwenye maisha ya kawaida wasichana 82 wa Chibok waliookolewa hivi karibuni kutoka kwa kundi la Boko Haram imeanza.

    Waziri wa wanawake na maendeleo ya jamii Bibi Aisha Alhassan amesema wasichana hao watapata matibabu ya kisaikolojia na dawa pamoja na mafunzo husika mjini Abuja, ili kuwasaidia wajiunge kwenye jamii na kurudi tena kwenye maisha ya kawaida.

    Wasichana hao 82 waliokuwa chini ya ulinzi wa polisi wa Nigeria wamefanyiwa upimaji wa mwili, kukutana na familia zao na sasa wako tayari kupelekwa kwenye vituo vya marekebisho ili wasaidiwe.

    Wasichana zaidi ya 200 walitekwa nyara na kundi la kigaidi la Boko Haram mwezi Aprili mwaka 2014 mjini Chibok, kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno, wasichana 82 kati yao waliokolewa mwanzoni mwa mwezi Mei.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako