Rais wa Marekani aondoa nchi yake katika makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi
Rais Donald Trump ametangaza kujiondoa kwa Marekani katika makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi uliotiwa saini mwaka 2015.
Amesema mkataba huo si wa haki na unahatarisha mamilioni ya nafasi za kazi za watu wa Marekani.
Kujitoa katika mkataba huo ilikua ni mojawapo ya ajenda wakati wa kampeni za Trump
Bw Trump amesema yuko tayari kuanzisha mashauriano ya mkataba mpya au airejeshe Marekani baadaye katika mkataba huo chini ya masharti yaliyoimarishwa.
Lakini amesema kuwa yeye hawezi kuunga mkono makubaliano ambayo - kwa matamshi yake mwenyewe - yanaadhibu Marekani bila kuwawajibisha wachafuzi wakubwa wa mazingira, ambapo amezitaja China na India.
Bw Trump amesema wakati wa kampeni za urais mwaka jana, aliahidi kwamba angechukua hatua kusaidia sekta za mafuta na makaa yam awe nchini Marekani.
Wapinzani wake wanasema kujiondoa kwenye Mkataba huo ni sawa na Marekani kuyakimbia majukumu yake kama kiongozi katika kukabili changamoto hiyo inayoikabili dunia.
Mkataba wa Paris unaitaka Marekani na nchi nyingine 187 kudhibiti ongezeko la viwango vya joto duniani kuhakikisha kiwango cha joto kinafikia nyuzijoto 2C chini ya kiwango kilichokuwepo kabla ya mageuzi ya kiviwanda, na baadaye kukipunguza zaidi hadi nyuzijoto 1.5C.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |