Sudan Kusini yaanza kusikiliza kesi ya askari wanaotuhumiwa kuwabaka wafanyakazi wa misaada
Jeshi la Sudan Kusini SPLA limeanza kusikiliza kesi dhidi ya askari 20 wanaotuhumiwa kuwabaka wafanyakazi wa misaada kutoka nje, kuwapora na kuwaua kwenye hoteli ya Terrain huko Juba wakati wa vurugu za Julai 11 mwaka jana.
Akiongea na wanahabari kuhusu kesi hiyo, kaimu msemaji wa SPLA kanali Santo Domic Chol amesema watuhumiwa 13 kati ya 20 wamefikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi, baada ya rais Salva Kiir kuamuru kufanyika uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo lililosababisha serikali kupata shinikizo kubwa kutoka nje, baada ya kugundulika kuwa wengi wa wahanga ni raia wa Marekani.
Msemaji huyo ameongeza kuwa waathirika na mashahidi hawatatoa ushahidi mahakamani isipokuwa meneja wa hoteli Michael Woodward, ambapo ushahidi wake wa awali ulionesha kuwa kati ya askari 50 na 100 walivamia eneo la hoteli baada ya kuwazidi nguvu walinzi wa usalama na kukaa kwa saa 72 wakifanya uhalifu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |